Huduma za Biashara
Timu yetu ya wataalamu wenye uzoefu wamezindua miradi yenye matokeo mazuri katika nyanja za Mawasiliano, Fedha, na Teknolojia. Tunapanga, tunakamilisha, na kutekeleza miradi barani Afrika.
Tuna uzoefu mkubwa katika Sekta ya utoaji Mikopo kwa Watumishi wa Umma.
Tumejikita katika maeneo yafuatayo;
Bidhaa za Biashara
Tunasaidia mashirika katika sekta ya kifedha, mawasiliano, bima, na rejareja katika mchakato wa kubuni, kuunda, na kuzindua bidhaa za watumiaji.
Kuanzia hatua ya mwanzo hadi ya mwisho wa utoaji mikopo. Tunasaidia mashirika katika kufafanua na kuboresha mchakato wa uombaji mikopo, ukaguzi, idhini, kuwasilisha nyaraka, na mchakato wa ukusanyaji deni, tukisisitiza umuhimu wa kasi kwenye utoaji wa mikopo (TAT) wakati tukitekeleza udhibiti ili kuepusha utoaji mikopo batilifu.
Kuandaa rasilimali. Kwa msaada wa idara yako ya rasilimali watu, tunasaidia katika kutambua na kuajiri rasilimali zinazoweza kufaa kwa shughuli za field, maafisa wa mbele na nyuma ya ofisi, na maafisa wa kusimamia uendeshaji wa kila siku wa mradi.
Ukuaji. Tunasaidia kutambulisha mifumo thabiti ya utoaji mikopo, kuboresha na kuautomate processes, kukuza na kuweka mifumo kwenye njia zako za usambazaji ili kuwezesha kuwafikia wateja, na hatimaye kuongeza mapato ya biashara yako.
Uwakala na Usambazaji
Ujuzi wetu katika usambazaji wa bidhaa unatutofautisha na washindani katika nafasi ya Mikopo kwa Wateja.
Tunatoa huduma za wakala kwa taasisi za kifedha kwa kuajiri, kutoa mafunzo, na kuingia field ili kuandikisha mikopo na bidhaa za bima kwa niaba ya wateja wetu.
Timu yetu ya Washauri wa Uuzaji (Mawakala) wamepata mafunzo vizuri na wamejengewa uwezo wa kutosha kuweza kutoa huduma zinazohitajika.
Maafisa mikopo wanajukumu muhimu katika kukagua maombi ya awali ya mikopo yanayopokelewa kutoka kwa timu zetu walio field, kuhakikisha maombi yanakidhi mahitaji kabla ya kuwasilisha kwa taasisi ya kifedha kwa mchakato wa mwisho.